NIA NA MADHUMUNI
Ili kuboresha kanzi data yake, Mahakama inatangaza nafasi za kazi kwa wakalimani wa kujitegemea wenye sifa zinazostahili katika lugha ya Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kihispania na Kiswahili ambao ni raia wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.
Zingatia: Wale ambao wametuma maombi hapo awali na kujulishwa kuwa wamefaulu kujumuishwa kwenye kanzidata hawahitaji kutuma maombi tena
WIGO
Wakalimani wa kujitegmea wanaalikwa kuonyesha nia ya kutoa huduma kwa njia ya mtandao na ana kwa ana (kwa mfano, wakati wa vikao na mikutano mingineyo ya Mahakama). Watapewa mikataba ya kutoa huduma za ukalimani kwenye mikutano iliyoandaliwa na itakayoandaliwa na ofisi ya Msajili wa Makama
Deadline: 03 May 2023