NIA NA MADHUMUNI:
Ili kuboresha kanzidata yake, Mahakama inatangaza na fasi za kazi kwa wafasiri wahariri wenye sifa zinazostahili ambao ni raia wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika wenye lugha za Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kihispania na Kiswahili kutuma maombi yao.
Zingatia: Wale ambao wametuma maombi hapo awali na kujulishwa kuwa wamefaulu kujumuishwa kwenye kanzidata hawahitaji kutuma maombi tena.
WIGO:
Wafasiri wahariri wa kujitegemea wanaalikwa kuonesha nia ya kutoa huduma ya ana kwa ana na kwa njia ya mtandao (kwa mfano, wakati wa vikao na mikutano ya Mahakama). Watapewa mikataba kwa ajili ya ufasiri na uhariri wa nyaraka za Mahakama.
Deadline: 03 May 2023